Thursday, January 10, 2013

WELCOME - KARIBU

Kikundi cha sanaa Kirumba (Kirumba Sanaa Group) kama kinavyojulikana ni kikundi chenye kulenga kuinua vipaji vya wasanii wachanga na kuleta changamoto chanya katika ukuzaji vipaji, Sanaa na Utamaduni katika Mkoa wa Mwanza na Tanzania kwa jumla.



Dira
Kirumba Sanaa Group tumeazimia kujenga uwezo na kuwa kikundi cha sanaa chenye nguvu si Mkoani Mwanza pekee au Tanzania bali kimataifa.

Malengo
Kuwajengea vijana wenye vipaji uwezo wa kujitegemea kupitia fani mbalimbali za sanaa na ufundi na hili ndilo lengo kuu la kuanzishwa kwa kikundi hiki. Na hii itakuwa changamoto kwa wadau wengine katika kupambana na umaskini uliokithiri katika jamii yetu. Hivyo basi tumekusudia kuwapa wahitaji nyavu badala ya samaki. Na tunaamini kwamba malengo haya yatafikiwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali

Tazama Tamthilia ya Malimwengu hapa - Watch Malimwengu Drama DEMO (IPO TAYARI KWA SOKO SEHEMU 39 ZIMEKAMILIKA IKIWA NI PAMOJA NA KUHARIRIWA KATI YA 52 NA JUMLA YA SEHEMU 26 ZIMESHAPIGWA PICHA BADO UHARIRI UNAENDELEA) Sehemu mojawapo kinahusu usafi wa mazingira na afya.



Bofya chini kwa maelezo zaidi

Pata habari mbalimbali na matukio


Mchezo wa Radio uitwao Yaleyale upo hatua za mwisho kukujia wakati Tamthilia ya Malimwengu ikizidi kukolezwa vionjo na chumvi na pia unaweza ku-sakinisha (download) wimbo wa yaleyale ambao umeimbwa na wasanii wa KSG (Amina "Emmy" Sango aka Kibeku, Jonas aka Mafuru na Athumani Sanifu aka Wembe)


Mtunzi na baadhi ya washiriki wa mchezo uitwao YALEYALE


  Picha za baadhi ya wahusika wa Tamthilia ya Malimwengu


Shime na Karenga wakiwa wadogo

Shime na Karenga katika utu uzima wao!

Huyu ni FUKUFUKU!


Mtendaji - Kunenge akiwa katika pozi



Kirumba Sanaa Ilitembelewa na Wageni Hawa:

Bwana Hashim Kambi Msanii maarufu Tanzania akiwa na BABA SAFURA

Msanii Maarufu Tanzania Adam Melele almaarufu SWEBE akiwa na Msanii mwenzake Katumba

Msanii SWEBE akiwa na Msanii Amon na wasanii chipukizi

Mwanza kumbe ni patulivu usiku....

 

No comments: