Baadhi ya Vipande vya Tamthilia ya Malimwengu kutoka Kirumba Sanaa Group itakayokujia hivi karibuni katika kituo maarufu cha Televisheni - Kaa mkao wa kuiona. Tamthilia hii ina zaidi ya unachokiona hapo. Inafurahisha, kufundisha, kuliwaza na kuonesha ukomo wa uvumilivu.
Picha za baadhi ya matukio na wasanii wanaoshiriki uchukuaji picha wa TAMTHILIA inayoandaliwa na Kikundi cha Sanaa Kirumba. (usiwe na shaka kaa mkao wa kula.... ikishaiva utapata jina na kituo itakachorukia.... lakini chumvi na ladha utavionja hapa. Karibu sana na tunawaomba muwe nasi kwa ushauri na michango yenu ya aina mbalimbali. Ahsanteni)
He! Jamani kule kijijini kumbe mbali... toka kule mpaka hapa!
Mnaujua huu mti nyie wajukuu zangu?
Huyu jamaa kama nilishawahi kumuona! "Washkaji ngojeni kwanza nipumue dah!"
Hii haiwezekani kabisa hata sikubali mpaka niujue ukweli....
Hivi babu hali ya hapa kijijini wewe unaionaje?
Julius Mahela kutoka Sabaktan Multimedia akipiga kazi kijijini katika maandalizi ya uchukuaji Tamthilia, akisaidiwa na msanii wa KSG Athumani Sanifu aliyevaa kofia ya babu!
Kwa matatizo yoote ya utabiri wa hali ya hewa, kiafya, biashara, bahati kutafuta wachumba huyu jamaa alikuwepo
Mandhari zilikuwa za kuvutia sana.... hususan miamba na mapango.
"mie nasubiria msosi tu hapa saa hizi.... kwani zamu yangu kuigiza tayari?"
"Aaaah mie kawaida kwenye ugomvi huwa sisogei.... nakaa mbali na kujitazamia tu"
Sijui kwanini watu huwa wanakimbia maisha ya vijijini lakini ni poa kweli...
Imebidi nivae miwani ili kuona unachokiangalia.....
"Yani hata kukusuka mpaka nikubembeleze? Nywele zako zangu? au unadhani kuna umeme hapa!
Mandhari zilikuwa za kuvutia sana na ni vivutio kwa utalii zikiwekwa wazi...
we weita maji nimeshakunywa niletee na juice ya ubuyu fasta
"Dada hebu kaa vizuri tuchukue na shot hii..." anaonekana Mr. Mahela akimwambia msanii wa KSG. Shukrani za dhati ziwaendee Afrimak waliotufadhili ofisi kwa ajili ya kuchukua vipande vya tamthilia yetu na pia ushauri wao kwetu ulikuwa wa tija.
"we sista vipi? weka mikono hivi...." anaonekana Mr. Ben akimuelekeza msanii wa KSG
Katibu KSG akiwa na msanii maarufu kama SWEBE ambae ni mdau katika sanaa.
Viongozi na Wasanii KSG wakishiriki msiba wa baba wa msanii Tufaa
Hapa ndipo mambo yalipoharibika walikwenda kumuona mgonjwa na kukuta amefariki!
Baba Safura katika picha ya pamoja na wanae... (familia hii nyie acheni tu!!)
Tamthilia yenu itakuwa tayari lini wakuu?
ReplyDeleteMkuu kaa mkao wa kula kazi inaelekea ukingoni na matokeo tutawawekea hapa hivi karibuni - Admin
ReplyDelete